Latest Posts

WAGONJWA WASIOJIWEZA KUSAIDIWA GHARAMA ZA MATIBABU

Shirika lisilo la kiserikali la Pearable Good Samaritan Tanzania Organization (PGST) limeanzisha mpango maalum wa kuwasaidia Watanzania wanaokabiliwa na changamoto ya gharama za matibabu hususani wale wasiokuwa na uwezo wa kugharamia huduma za afya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Mwanza, Katibu na Mkurugenzi wa Oparesheni wa PGST, Josephat Fidelis Swai amesema shirika hilo limejipanga kuwafikia watu wanaougua lakini hawajui namna ya kupata msaada wa kifedha kwa ajili ya matibabu.

“Kumekuwa na Watanzania ambao wanaugua kwa kupata maradhi au changamoto za kimaradhi lakini hawajui ni namna gani wataweza kuzikabili gharama za matibabu jambo hilo linapelekea wengine kukata tamaaa, kutelekezwa na hata ndugu, jamaa na marafiki,” amesema.

Kwa mujibu wa Swai, baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakitumia matatizo yao kama njia ya kuomba misaada mitaani kwa kushika fomu za uchangishaji na kuomba msaada, hata hivyo wamekuwa wakishindwa kufikia gharama za matibabu yao huku kwa upande wa jamii wakikosa uaminifu.

“Jambo hilo limekuwa kama fursa kwa baadhi ya watu wenye maradhi au magonjwa kuchukulia kama ni sehemu ya kujipatia kipato unakuta mtu anazunguka na fomu ya uchangishaji kweli anaugua ana maradhi lakini anapopatiwa kile kiasi cha fedha kwa ajili ya kwenda kutatua changamoto hiyo anakosa uaminifu,” amesema Swai

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!