Latest Posts

WALIMU WAASWA KUACHANA NA MIKOPO ‘KAUSHA DAMU’

Na Mwajuma Hassan, Iringa

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amewataka walimu kuachana mara moja na tabia ya kukopa fedha kutoka kwa watu binafsi na vikundi visivyo rasmi vinavyotoa mikopo kwa masharti kandamizi maarufu kama “mikopo kausha damu”.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito huo katika kongamano la walimu  lilioandaliwa na   Benki ya NMB ambapo amesema  kuwa mikopo isiyo rasmi imekuwa chanzo cha migogoro, msongo wa mawazo, na hata migogoro ya kifamilia kwa baadhi ya walimu.

“Mwalimu anatakiwa kuwa na nidhamu ya fedha. Tuachane kabisa na mikopo yenye masharti kandamizi. Tumieni taasisi rasmi kama benki hii ya NMB na SACCOS zilizosajiliwa ambazo zinatoa mikopo kwa masharti nafuu na salama,” alisema Kheri James.

Aliongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na taasisi za kifedha kama Benki ya NMB ili kuwawezesha walimu kupata mikopo rafiki itakayowasaidia kuinua hali yao ya maisha bila kuwaweka kwenye madeni yasiyoisha.

Kwa upande wake, Meneja mauzo NMB kanda ya nyanda za juu kusini Manyilizu Masanja alisema kuwa benki hiyo imekuwa mshirika mkubwa wa sekta ya elimu kwa kutoa huduma mahususi kwa walimu kupitia mpango wa Mwalimu Spesho.

“Mpango huu unazingatia hali halisi ya kipato cha walimu. Tunatoa mikopo yenye riba nafuu, muda mrefu wa marejesho, na ushauri wa kifedha kwa kila mkopaji,” alisema meneja huyo.

Amesema elimu hiyo inalenga kuwawezesha walimu kuwa na maarifa yakufanya maamuzi sahihi yakifedha  kwa ajili ya ustawi wao wasasa na maisha ya baada ya kustaafu.

Mmoja wa walimu waliohudhuria kongamano hilo , Mwalimu Majid Mbeju kutoka shule ya msingi zizi , amesema  kuwa mikopo ya mtaani imewaacha walimu wengi wakiwa na madeni yasiyoisha na kukosa amani kazini na nyumbani.

“Mikopo ya watu binafsi ni ya haraka, lakini inavunja maisha ya walimu wengi,wengi wetu hatuna elimu ya kifedha ,hivyo Tunaishukuru benki ya NMB kwakutufikia na kutupa mbinu zakujikwamua kiuchumi,” alisema.

Kwa sasa, taasisi mbalimbali za kifedha zinaendelea kuhamasisha walimu kujiunga na vyama vya akiba na mikopo (SACCOS), pamoja na kutumia huduma za benki rasmi ili kuepuka mitego ya kifedha isiyo rasmi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!