Latest Posts

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA CHINA

Jumuiya ya Watanzania waishio nchini China (DITAG) imetoa wito kwa wafanyabiashara wa Tanzania kuchangamkia fursa mpya ya kibiashara kufuatia hatua ya kuruhusu mazao 14 kuingizwa nchini China bila ushuru wa forodha.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Tarehe 16 Julai 2025, Katibu Mkuu wa DITAG, Ndugu Alawi Abdallah, amesema kuwa fursa hiyo ya kipekee ni matokeo ya uongozi bora na mahusiano ya kidiplomasia yaliyoimarishwa kati ya Tanzania na China chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa Alawi, mazao yaliyopata kibali rasmi kuingia China bila kulipiwa ushuru wa forodha ni pamoja na: Parachichi, Ufuta, Mihogo mikavu, Asali, Pilipili, Mbegu za pamba, Alizeti, Kahawa (iliyokaangwa na isiyokaangwa Karafuu, Pembe za ng’ombe

Ameeleza kuwa mazao mengine yako katika hatua za mwisho za tathmini na yanatarajiwa kuidhinishwa muda wowote kuanzia sasa.

“Hii ni fursa ya kipekee kwa wakulima na wafanyabiashara wa Tanzania kupeleka bidhaa China bila kulipa kodi. Tunawahamasisha Watanzania kuitumia ipasavyo,” alisema Alawi.

Aidha, amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mpango wa DITAG wa kuhakikisha usalama, uaminifu na faida kubwa kwa Watanzania wanaojihusisha na biashara ya kimataifa, pamoja na kuanzisha mfumo rasmi wa uhakiki wa waagizaji ili kulinda maslahi ya wauzaji wa bidhaa kutoka Tanzania.

DITAG imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwaunganisha wafanyabiashara wa pande zote mbili na kutoa mwongozo wa kitaalamu kwa watakaotaka kunufaika na soko hilo lenye mahitaji makubwa ya bidhaa kutoka Afrika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!