Latest Posts

WITO WATOLEWA KWA WANANCHI KUFANYA VIPIMO VYA MACHO MARA KWA MARA

Wananchi kote nchini wametakiwa kuweka utaratibu wa kupima macho mara kwa mara ili kubaini mapema matatizo yanayoweza kuathiri uwezo wao wa kuona na kupata matibabu kwa wakati kabla hali haijawa mbaya.

Wito huo umetolewa na Rais wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Macho na Wataalamu wa Macho Tanzania, Dkt. Christopher Evarist, wakati wa mkutano wa kitaifa wa wataalamu wa macho uliofanyika jijini Mwanza kwa siku mbili, ukiwaleta pamoja wataalamu wa macho kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema changamoto za macho bado ni kubwa nchini na zinagusa karibu makundi yote—watoto, vijana na wazee.

Kwa upande wake, mgeni rasmi wa mkutano huo ambaye pia ni mdau mkubwa wa huduma za afya ya macho, Lias Habil Khanbhai, alitoa rai kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na serikali na mashirika binafsi katika kuimarisha huduma za macho.

Kaulimbiu: Ushirikiano wa Sekta Binafsi na Umma

Mkutano huo uliongozwa na kaulimbiu isemayo: “Public Private Partnerships for Eye Health: Driving Sustainable Impact in Tanzania” ikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi katika kuhakikisha huduma za macho zinaboreshwa na kuwa endelevu.

 

Dkt. Evarist alisema mkutano huo umetoa fursa kwa wataalamu kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto zinazowakabili katika kutoa huduma, na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kufikia Watanzania wengi zaidi wanaohitaji huduma za macho.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!