Na Helena Magabe -Tarime.
‎Nyambari Chacha Mariba Nyangwine si mgeni masikioni mwa watu wengi Nchini hasa Mkoa wa Mara , ni Mzaliwa wa Wilayani Tarime Mkoani Mara,ni mtunzi na mchapishaji wa vitabu,lakini pia ni mfanyabiashara mkubwa aliyewekeza miradi yake mbalimbali ndani ya Nchi  pamoja na nje ya Nchi ikiwemo Uganda,Congo,Dubai pamoja na kwingineko.
‎Nyangwine aliwahi kuwa Mbunge wa Tarime 2010-2015 wakati huo Tarime ilikuwa na jimbo moja ,kwa sasa ni mtia nia anayewania kugombea jimbo la Tarime Vijijini huku nyota yake ikionekana kung’ara zaidi kuliko watiana wenzake waliojitokeza kuwania jimbo hilo.
‎Nyangwine (CCM) mwaka huo 2010 alishindana  na Mwita Mwikwabe Waitara kipindi hicho akiwa upinzani (CHADEMA ) alimshinda mpinzani wake huyo na kufanikiwa kuutwaa ubunge wa Jimbo la Tarime, baada ya kumaliza muda wake jimbo liligawanywa na kupata majimbo mawili Tarime Viijijini pamoja na Mjini.
‎
‎2015 -2020 safari hii upepo uligeukia upinzani John Heche(CHADEMA) akatwaa Tarime Vijijini huku Esther Matiko(CHADEMA) kwa sasa CCM akatwaa jimbo la Tarime Mjini Mwita Waitara akagombea Ukonga Dare es salaam jimbo likiwa moja akashinda na kutwaa ubunge 2015-2020.
‎Nyangwine alipumzika na kuendelea na shughuli nyingine kama wafanyavyo wanasiasa wengine ni jambo la kawaida kabisa kwa mwanasiasa kupumzika ama kuhama chama ,Mwita Waitara akarudi teba CCM akagombea Jimbo la Tarime vijijini akipambana na mpinzani John Heche lakini Waitara akafanikiwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo la TarimeVijijini , anaelekea kumaliza muda wake huku akiwania tena ubunge kwani amekwisha tia nia akiwa miongoni mwa watia 12.
‎Baada ya kufanya utafiti na kuwaletea makala ya Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Eliakimu Maswi na kubaini kiongozi huyo alivyokuwa kipenzi cha Wananchi wa Jimbo la Tarime Vijijini ,sasa nimekuja na tafiti ya Nyambari Nyangwine ambaye alikuwa akimfatia kutamba katika mitandao ya kijamii, ni wazi kwamba jina hilo likifanikiwa kurudi kuna uwezekano mkubwa wa kutwaa jimbo hilo kwa mara nyingine tena ingawa Dkt Edward Machage naye anaoneka kutajwatajwa.
‎kulikuwa na mchuano mkali kwenye mitandao ya kijamii dhidi ya Wafuasi wa Maswi,Nyangwine pamoja na Waitara inasemekana kuwa Mtu pekee aliyekuwa akiwanyima usingizi watinia wengine ni Maswi kutoka na kuwa na nguvu na wafuasi wengi ,licha ya kuwa alikuwa hajatamka popote kuwa anagombea lakini minong’ona ya watu wake wa karibu ilitapakaa na kufanya majina hayo matatu kuskika zaidi kwenye mitandao ya kijamii na kwa Wananchi.
‎Sasa ni zamu ya Nyangwine kung’ara baada ya kuchukua nafasi ya Maswi kwani kwa sasa anatamba mitandaoni na wafuasi wake wanaonekana wenye nguvu zaidi kuzidi kuliko wafuasi wa watiania wengine , licha ya hilo Nyangwine anaonekana kuwa na wafuasi wengi kuliko watinia wengine.
‎Kwanini Nyangwine anarudi, kwanza kwanini anakubalika kuna mambo mengi mazuri alifanya akaacha alama na mengine yameshindwa kumaliziwa na waliomfatia hivyo anarudi ili aendeleze yaliyofanyika na yaliyokwama amalizie, aliyoyafanya ni mengi ili nitawapitisha kwenye machache kati ya hayo ili muweze kufahamu kwa wale ambao hamkubahatika kufahamu.
‎Nguri huyu  mtunzi na mzalishaji wa Vitabu vya shule ya msingi na Sekondari, kwanza kabisa ikumbukwe alishiriki mchakato wa uanzishwaji wa Halmashauri ya Tarime Vijijini pamoja na Tarime Mjini pamoja na uazishwaji wa makao makuu ya Halmashauri ya Vijijini katika kata ya Nyamwaga na leo hii Halmashauri hiyo ya Vijini iko huko.
‎Kwa kuwa ni mdau mkubwa wa elimu alifanikisha kuwepo na ongezeko la shule toka shule 14 -38, aligawa vifaa vya michezo kwa wanafunzi pamoja na timu za Vijana vile vile hakusita kugawa vitabu alivyovizalisha ambapo aligawa vitabu kwa shule za msingi na sekondari vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.
‎Aliwahi kugawa mabati 6,000 yaliyotolewa na Hifadhi ya Wanyama TANAPA kutokana na mahusiano mazuri ambapo yalitumika kwenye baadhi ya Shule, zahanati pamoja na Vituo vya Polisi,si hayo tu alishiriki na kufanikisha soko la Kimataifa Remagwe ambalo likiisha litakuwa kitovu cha biashara kati ya Nchi jirani ya Kenya na Tanzania.
‎licha ya kuwa yapo mengi nikomee kwenye uazishwaji wa barabara ya rami Nyamwaga -Nyamongo ambayo hadi leo inajengwa kiduchu kiduchu pengine labda ndiyo inayomsukuma zaidi kurudi ili aimalizie .
‎Mpaka kufikia hapo nina imani msomaji wangu umepata kumwelewa Nyangwine ambaye ana maono na matamanio ya kuhakikisha anabadirisha taswira ya Jimbo la Tarime kwa kuleta maendeleo makubwa ya kisekta,ana utashi wakuleta mabadiriko kwenye maisha ya Watu wa jimbo hilo pamoja na kuleta ustawi endelevu.
‎Bila kumsahau kijana Msomi Marwason Migera aliyetia nia ya udiwani anaunga juhudi za Nyangwine huku akipata sapoti kubwa toka kwa wafuasi wake ambao wengi ni vijana ambao kwa nyakati tofauti wamebaisha kuwa ushindi sasa ni wake Nyangwine .
‎Mzee mmoja Mkazi wa Nyamwaga ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema Jamii inampenda Nyangwine katika Kijiji chake cha Nyamwaga kata ya Nyamwaga, lakini hajui jina litakalorudishwa baada ya mchujo kwani hajui nani atarudi katika mchujo huo utakaoleta majina matatu yatayopigiwa kura.
‎Ghati Mtera Mkazi wa Nyarero alisema Nyambari amewekeza sana kwa Mungu kwa kuchangia makabisa mengi katika harambee na hakuna aliyetoa kwa Mungu akapungukiwa pengine ndio maana ana watu wengi wanaomuunga mkono vijana kwa wazee na kina mama.