Latest Posts

EU YAMKOSOA BALOZI WAKE TANZANIA KWA UKIMYA DHIDI YA KESI YA LISSU

Bunge la Ulaya limekosoa vikali ukimya wa Balozi wake nchini Tanzania, Bi Christine Grau, kufuatia kile walichokitaja kuwa ukandamizaji wa kisiasa unaomkabili kiongozi wa upinzani, Tundu Lissu.

Katika kikao cha Kamati Ndogo ya Haki za Binadamu (DROI) kwa kushirikiana na ujumbe wa Bunge la Afrika-EU na ule wa OACPS-EU, kilichofanyika siku ya Jumanne, Mbunge wa Bunge la Ulaya, Bw. Michael Gahler, alisema hatua ya balozi Grau kutochukua msimamo kuhusu hali ya Lissu ni jambo lisilokubalika.

Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi kumkosoa Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Dk. Constantinos Kombos, aliyefanya ziara rasmi nchini Tanzania hivi karibuni, kwa kile alichokiita “kusifia hali ya kisiasa nchini pasipo kuangalia ukweli halisi wa mambo”.

“Ni aibu kuona kiongozi kutoka Umoja wa Ulaya akisifia hali ya kisiasa Tanzania ilhali upinzani unanyimwa haki na wanasiasa wanazuiwa kushiriki uchaguzi huru,” aliongeza.

Bunge hilo limetoa wito kwa wawakilishi wake barani Afrika kutokuwa watazamaji wa kimya katika mazingira yoyote ya uvunjifu wa haki, hasa yanapowahusu wapinzani wa kisiasa na wanaharakati.

Ziara ya Dk. Kombos nchini Tanzania ilikuwa kwa niaba ya Mkuu wa Sera za Mambo ya Nje wa EU, Bw. Kaja Kallas, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika masuala ya kikanda na kimataifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!