Latest Posts

MAREKANI YATOA NYARAKA ZA SIRI ZA MAUAJI YA MARTIN LUTHER KING JR

Serikali ya Marekani kufuatia agizo la Rais wa Marekani Donald Trump, imetoa msururu wa nyaraka zinazohusiana na mauaji ya Martin Luther King Jr., kiongozi wa vuguvugu la haki za kiraia huko Marekani, zikiwemo nyaraka za uchunguzi wa FBI kuhusu mtu huyo mashuhuri katika historia ya Wamarekani wenye asili ya Afrika.

Nyaraka hizo za FBI zimezuiwa kutolewa hadharani kwa amri ya mahakama tangu 1977. Nyaraka hizo zina kurasa 230,000.

Wanafamilia wa King walipinga kutolewa kwa nyaraka hizo. Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu na watoto wawili wa Martin Luther King, wamelaani “matumizi yoyote mabaya ya nyaraka hizo kudhoofisha urathi wa baba yao.”

King, mchungaji wa Marekani na mwanaharakati wa haki za kiraia, alipigwa risasi na kuuawa huko Memphis Aprili 4, 1968, akiwa na umri wa miaka 39. James Earl Ray, mhalifu aliyepatikana na hatia, alikiri kufanya mauaji, lakini baadaye akaghairi kukiri kwake.

Siku ya Jumatatu, watoto wawili wa Martin Luther King Jr., Martin III na Bernice, ambao waliarifiwa mapema juu ya kutolewa kwa nyaraka hizo, walisema katika taarifa:

“Tunawahimiza wale wanaoshughulikia nyaraka hizi kuzishughulikia kwa huruma, kujizuia kuzitoa na kuheshimu huzuni isiyoisha ya familia yetu. Kutolewa kwa nyaraka hizi lazima kutazamwe katika muktadha kamili wa kihistoria.”

“Wakati wa uhai wa baba yetu, alilengwa sana kwa kampeni ya habari za kupotosha na ufuatiliaji ambao ulikuwa mkubwa, uvamizi wa faragha yake, na wa kusumbuliwa sana, hayo yakiongozwa na J. Edgar Hoover, mkurugenzi wa kwanza wa shirika la FBI, kupitia Idara ya Haki.”

Taarifa hiyo inasema ufuatiliaji wa serikali ulisababisha “ukiukwaji wa faragha” na “mashambulizi ya makusudi dhidi ya ukweli” ambayo yalimnyima Martin Luther King utu na uhuru kama raia wa kawaida.

Wakati wa kampeni za uchaguzi Novemba mwaka jana, Donald Trump aliwaahidi wafuasi wake ikiwa atashinda, atatoa nyaraka zinazohusiana na mauaji ya Martin Luther King, Jr. na Rais wa zamani wa Marekani John F. Kennedy.

Mwezi Januari, alitia saini agizo la kufichuliwa nyaraka zinazohusiana na mauaji ya wote mawili.

Trump amekuwa chini ya shinikizo katika wiki za hivi majuzi kuachilia ripoti kamili kuhusu Jeffrey Epstein, tajiri na mnyanyasi sugu wa kingono aliyejiua gerezani, ombi ambalo Trump na Mwanasheria Mkuu wake, Pam Bundy, bado hawajalikubali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!