Latest Posts

MAPIGANO YAZUKA TENA MPAKA WA THAILAND NA CAMBODIA, WANANCHI WATAHADHARISHWA KUHAMA

Mapigano ya risasi yameripotiwa kati ya wanajeshi wa Thailand na Cambodia katika eneo la mpaka unaozozaniwa, huku kila upande ukimshtumu mwenzake kwa kuanzisha mashambulizi.

Kwa mujibu wa BBC, hali ya taharuki imetanda huku wanavijiji waliopo maeneo ya karibu wakihamishwa kwa usalama wao.

Jeshi la Thailand limesema lililazimika kufyatua risasi baada ya kukutana na kundi la wanajeshi wa Cambodia waliokuwa na silaha upande wa mpaka. Hata hivyo, jeshi la Cambodia limekanusha madai hayo na kudai kuwa Thailand ndio iliyoanzisha mashambulizi hayo ya kwanza.

Mzozo huu wa karibuni unakuja siku chache tu baada ya uhusiano wa kidiplomasia kuzorota kufuatia uamuzi wa Thailand kumfukuza balozi wa Cambodia, huku ikimwita nyumbani balozi wake kutoka Phnom Penh. Haya yalifuatia mlipuko wa bomu la ardhini uliomjeruhi mwanajeshi wa Thailand karibu na mpaka.

Kwa sasa, ubalozi wa Thailand nchini Cambodia umetangaza tahadhari kwa raia wake walioko nchini humo kuondoka mara moja, isipokuwa wale walio na sababu za dharura. Hatua hii inaashiria hofu ya kuongezeka kwa mapigano na kuathiri usalama wa raia wa kawaida.

Chanzo kingine cha mvutano kimehusishwa na tukio la hivi karibuni ambapo Waziri Mkuu wa zamani wa Cambodia, Hun Sen, anadaiwa kumwaibisha Waziri Mkuu wa Thailand, Paetongtarn Shinawatra, kwa kuvujisha mazungumzo ya simu ya faragha kuhusu mpaka huo. Tangu tukio hilo, uhusiano kati ya mataifa haya jirani umekuwa ukidorora kwa kasi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!