Nilikuwa na miaka 24 tu wakati moyo wangu ulipasuliwa vipande vipande na watu wawili ambao niliwategemea zaidi duniani mpenzi wangu wa miaka miwili na dada yangu wa damu. Ilikuwa ni siku ya Jumamosi jioni niliporudi nyumbani mapema kutoka kazini baada ya mkutano wetu kuahirishwa ghafla. Sikuwa nimewapa taarifa, na nadhani hiyo ndiyo iliyofanikisha kile kilichofuata.
Nilipoingia nyumbani kwangu, mlango ulikuwa haujafungwa kabisa. Sauti za kicheko na kelele za mahaba zilinifanya kuganda mlangoni. Moyo wangu ulianza kudunda kwa kasi, lakini sikutaka kuamini kilichokuwa kikitokea. Nilipotupa macho chumbani, sikuamini macho yangu mpenzi wangu akiwa kitandani na dada yangu mdogo ambaye nilimwacha aje akae nami kwa muda.
Nilipiga mayowe, nikaporomoka chini kwa maumivu ya moyo ambayo hayawezi kuelezeka kwa maneno. Mpenzi wangu alijaribu kuja kuniomba msamaha, lakini nilimkata kabisa. Dada yangu alilia na kusema ni shetani tu aliyewapitia. Sikuwa tayari kumsikiliza mtu yeyote. Siku hiyo nilijifungia chumbani kwangu na sikuongea na mtu kwa siku mbili mfululizo. Soma zaidi hapa.