“Nilikuwa na uhusiano wa karibu sana naye, kipindi bado hajawa mtu mkubwa. Tulikuwa tunapendana sana. Lakini nilipopata ujauzito, mambo yalibadilika ghafla,” alisema Rehema akiwa kwenye mahojiano ya moja kwa moja. “Nilitishwa, nilihamishwa kutoka Dar es Salaam hadi Musoma, nikaambiwa nisijaribu kusema lolote.”
Kulingana na simulizi yake, alikutana na mwanasiasa huyo miaka tisa iliyopita alipokuwa kwenye kampeni za ubunge. Alisema walikuwa wakionana mara kwa mara na hata kulala naye katika nyumba ya wageni moja jijini Mwanza. “Wakati huo aliahidi tutaoana, na hata nikapata mimba hakupinga mpaka pale jina lake lilipoanza kupanda kisiasa. Niligeuzwa adui.” Soma zaidi hapa.