Kabla ya mambo kuharibika, kila kitu kilionekana kwenda vizuri. Mapambo yalikuwa yamewekwa kwa ustadi, chakula na vinywaji vilikuwa vimetandazwa, na muziki wa taratibu ulikuwa ukicheza kwa mbali. Wazazi wa pande zote mbili walikuwa wamekaa sehemu ya heshima wakisubiri kutambulishana rasmi. Lakini mambo yalibadilika ghafla wakati mama wa bwana harusi mtarajiwa alipomuona mrembo aliyekuja kama mchumba wa mwanawe akielekea kutoa hotuba yake.
Kwa sekunde chache alikaa kimya akimtazama, kisha ghafla akasimama na kumtaja kwa jina tofauti na lile alilopewa. “Wewe ni Janet, siyo Aisha! Wewe ndiye yule mpangaji niliyekupangisha nyumba mtaa wa Kihonda na ukakimbia bila kulipa kodi ya miezi mitatu!” alifoka kwa hasira huku ukumbi mzima ukikaa kimya. Wageni walianza kunong’ona huku wakishangaa kilichokuwa kikiendelea. Soma zaidi hapa.