Latest Posts

WAOSHA MAGARI SHINYANGA WAPEWA ELIMU YA USALAMA BARABARANI

Vijana wanaojihusisha na shughuli za uoshaji magari (car wash) katika Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani, ikiwemo kupewa onyo la kuepuka kuendesha magari ya wateja bila kuwa na sifa za udereva.

Elimu hiyo imetolewa na Sajenti David Ndimila wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, ambaye amewataka vijana hao kuacha tabia ya kuendesha magari ya wateja, akieleza kuwa vitendo hivyo vimesababisha ajali na uharibifu wa mali mara kwa mara.

“Wengi wenu mnaendesha magari ya wateja bila kuwa na leseni. Hali hii inasababisha ajali, uharibifu wa magari na wakati mwingine kugonga watu au vitu, jambo linaloweza kupelekea majeruhi na hata vifo,” amesema Sajenti Ndimila.

Alisisitiza kuwa ni vyema vijana hao kuzingatia tahadhari hizo ili kulinda maisha yao na mali za wateja.

“Waosha magari wanapaswa kumaliza muda wao wa kazi wakiwa salama, na pia kuhakikisha vyombo vya moto vya wateja wao vinabaki salama,” aliongeza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!