-Asema hakuna Serikali inayopenda wananchi wake wapate shida
-Asisitiza Serikali hii ni sikivu adha za usafiri wa mwendokasi iko kwenye hatua za mwisho kumalizwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila ametembelea kituo cha mabasi ya mwendokasi cha kimara na kuwahakikishia wananchi kuwa ndani ya wiki hii mabasi ya mwendokasi yataongezwa kwenye njia hiyo ili kupunguza adha ya usafiri na kwamba serikali tayari imeshaingia makubaliano na kampuni binafsi
Ziara hiyo ya RC Chalamila aliyoifanya alfajiri ya leo Septemba mosi ni kufuatia serikali mkoani humo kubaini adha kubwa wanayoipata wananchi wanaotumia usafiri huo wa mwendokasi hususani wanaotokea maeneo ya mbezi na kimara kuelekea katikati ya jiji
Akizungumza wakati wa ziara hiyo RC Chalamila amesema kabla ya kumalizika wiki hii serikali imekusudia kuleta mabasi machache wakati wakitafuta suluhisho la kudumu pia amesema zaidi ya mabasi 200 yameshapakiwa kuja Dar es salaam kutoa huduma hiyo kupitia mkandarasi mpya
Aidha kutokana na ombi la wananchi waliojitokeza wakati wa ziara hiyo kutaka mabasi ya kawaida kuruhusiwa kupeleka wananchi katikati ya jiji kupitia njia ya mwendokasi ama njia ya kawaida isiokuwa ya mwendolasi RC Chalamila amewaahidi wananchi hao kuwa anafanyiakazi kwa haraka mpango wa mabasi ya kawaida yaongezeke lakini si kwa kutumia njia ya mwendokasi kwa kuwa mfumo wake hauruhusu kutumia mabasi ya kawaida
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliojitokeza wameiomba Serikali kusaidia kumaliza adha hiyo kwa kuleta mabasi ya kutosha lakini pia kwa kuruhusu mabasi ya kawaidi kuongezwa ili kurahisisha wananchi kufikishwa katikati ya jiji