Latest Posts

MABASI MAPYA YA MWENDOKASI YA KAMPUNI YA MOFAT YAANZA KUBEBA ABIRIA KUTOKA MBEZI, KIMARA

Mabasi mapya ya Mwendokasi ya Kampuni ya MOFAT leo Oktoba 02, 2025 yameanza kubeba abiria wa Mbezi Kimara ili kuondoa kero kubwa iliyokuwepo katika barabara hiyo ya upungufu pamoja na ubovu wa mabasi ya Mwendokasi.

Mabasi hayo yameanza kazi asubuhi hii ikiwa ni saa chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila atangaze jana ya kwamba kwa agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baadhi ya mabasi ya MOFAT ambayo ni maalum kwa njia ya Mbagala yatahamishiwa kwenye barabara ya Kimara ili kuondoa changamoto ya uhaba wa mabasi iliyopo kwa sasa.

Mabasi haya mapya leo yameanza kubeba abiria kwenye barabara ya mwendokasi kuanzia Kimara Mwisho kuelekea Gerezani, Kivukoni na Morocco.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!