Latest Posts

WANASIASA WATAKIWA KUKEMEA UKATILI WA KIJINSIA

Na Helena Magabe -Tarime

‎Wanasiasa wametakiwa kukemea ukatili wa kijinsia  hasa kwenye upande wa ukeketaji kwa Watoto wa kike na sio kufumbia macho na kuwa moja ya sehemu ya kuunga mkono kisirisiri ukeketaji kuendelea kuwefanyika kwa lengo la kuhofia kupoteza au kupunguza wapiga kura.

‎Hatua hiyo imekuja baada ya kufanyika mafunzo kwa Waandishi wa Habari   Wilayani Tarime  juu ya ukatili wa kijinsia ambapo Wanasiasa wameoneka kutajwa kuwa  sehemu ya kusababisha ukeketaji uendelee kufanyika   kwa kuhofia kupoteza nafasi walizonazo kwa kutopigiwa kura kuchaguliwa ili kuendelea kuwa Viongozi .

‎licha ya kuwa Wazee wa Mila na Mang’ariba mara kadhaa wamekuwa wakipewa semina elekezi juu ya madhara ya ukeketaji  na kuahidi kuachana na vitendo hivyo ,lakini ukeketaji bado unaendelea kufanyika kwa kubadirisha tu mfumo au njia  ya ukeketaji ili mradi kuendelea kutetea na kulinda mila huku Wanasiasa wakioneka kufumbia macho kwa kulinda mkate wao.

‎

‎Mkufunzi wa mafunzo ya ukeketaji na ndoa za utotoni James Massawe yaliyofanyika siku mbili Octoba 13-14 Wilayani  amewataka wanasiasa kuwa mstari wa mbele kupinga ukeketaji ambapo amesema licha ya wazee kuwa wagumu kuachana na ukeketaji ,chanzo kingine ni wanasiasa wanahofia kupoteza wapiga kura.

‎Massawe alisisitiza  waandishi kutosita kuandika habari za kuelimisha Jamii juu ya vitendo vya ukatili lakini wahakikishe wanatenda haki ,na kufata maadili ya uandishi wa habari pamoja na miiko huku akisisitisa washirikiane na wanasiasa na kuwa sehemu ya Jamii katika kupinga vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu.

‎Waandishi kutoka mikoa  mbali mbali walioshiriki mafunzo ya juu ya kuandika habari za ukatili wa kijinsia walielezea vikazo mbali mbali  wa navyo kutana navyo vinavyochangia ukatili kuendelea kufanyika huku wakiwataja Wanasiasa kuwa nao ni  chanzo cha kukwamisha ukeketaji kwani hawakemei kwenye majukwaa ukeketaji licha ya kuwa  wana nguvu na wanasikilizwa na Wananchi vile vile hawatoi ushirikiano kwa Waandishi juu ya swala la ukeketaji.

‎

‎Maoni  mbali mbali yaliyotolewa ni kwamba Wanasiasa wajitokeze hadharani kwenye majukwaa kumemea,Viongozi wa dini,mashirika yatoe ujuzi na ufundi stadi kwa watoto wa kike,Serikali isimamie sheria ya mtoto kikamilifu,elimu itolewe bila kuchoka kwa makundi ambayo hayataki kubadirika pamoja na Serikali kuweka mpango mkakati kwa Mtoto wa kike pindi anapomaliza shule akiwa hajafauru masomo yake.

‎Victor Maleko Mkufunzi kutoka UTPC umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania yeye alisisitiza ,maadili,haki na weledi katika kuandika habari za ukatili wa kijinsia ambapo alisema kumekuwa na uvunjifu wa haki katika kuandika habari za ukatili kwa kuvunja miiko ya habari na kutozingatia sheria ya kuandika habari za watoto chini ya miaka 18  pamoja na kwa wahanga wote wa ukatili wanaostahili kuhifadhiwa.

‎Alisema kumekuwa na uvunjwaji wa haki katika kuripoti habari za ukatili hali inayopelekea wahanga wa ukatili na jamii kukosa imani na Waandishi wa habari kwani wamekuwa wakiweka wazi yale yasiyostahili kuwekwa wazi, ambapo yanapelekea kuwavunja moyo kwa madhira waliyoyapitia badala ya kuwatia moyo na kuwatafutia suluhu badala yake wamekuwa sehemu yakuwaumiza mambo hayo ni kama kuwataja kwa majina ,kutowaficha sura na mengineyo.

‎Mkuu wa miradi katika shirika la Idadi ya Watu C-Sema ambao ndio waandaji wa  semina hiyo Michael Marwa alisema kuwa wametoa mafunzo rejea kwa Waandishi wa habari ili kuwakumbusha waandishi wa habari kuzingatia misingi ya kiuandishi inayozingatia haki za Binadamu ,utu na haki za waathirika wa ukatili wa kijinsia.

‎Alisema lengo ni kukumbushia na kufundisha utalamu wa kuandika habari za kijamii zinazoibua ukatili wa kijinsia kwenye jamii ili jamii inufaike na taaluma yao ya habari na kuonyesha utofauti wa kuripoti habari za ukatili kwa kuepuka kuvunja haki za binadamu na kuonyesha utofauti wa uandishi wa habari unaozingatia haki za Binadamu.na kuongeza kuwa shirika la UNFPA tangu 2021 limekuwa likifadhili shirika la C-sema kwaajili ya kutoa semina za ukatili wa kijinsia.

‎Afisa ustawi wa Jamii Siwema Silversta ambaye alikuwa Mgeni rasmi alisema,Waandishi wana haki na waajibu kulinda haki na ustawi wa Mtoto wa kike kwa kuibua matukio mbali mbali ya ukatili wa kijinsia ,haki za watoto wa kike pamoja na walemavu .

‎Waandishi wa habari kwa nyakati tofauti waliomba  elimu itolewe vijijini bila kukoma ambapo Dinna Maningo alishauri mikutano ya hadhara itumike kutoa elimu ambapo watawapata wahusika wote wanaunga mkono ukeketaji lakini mashirika yaendelea kutoa  elimu kwani  kutoa elimu kwa kundi la wazee wachache wa Mila elimu haitawafikia walengwa wote.

‎Kiongozi mmoja wa Kisiasa ambaye anagombea Udiwani kwenye Kata moja wapo Tarime Vijijini ambaye ameomba asitajwe jina lake wala kata yake alipopigiwa simu na Jambo tv kuhusu kukalia kimya ukeketaji alisema hawezi kuingilia mila ambayo ameiluta navyeye anaitekeleza ni swala gumu ,vile vile anaogopa wazee wa mila.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!