Taasisi ya Nyansaho Foundation imekabidhi Mchele kilo 900 na sukari kg 375 pamoja na mafuta ya kupikia na soda na chumvi katika vituo 19 vya Mkoa wa Mara vinavyolea watoto wenye mahitaji Maalum, Wazee, pamoja na Nyumba Salama.
Akizungumza mratibu wa Taasisi hiyo Modest Michael amesema wametoa Mchele,mafuta, chumvi soda,fedha taslimu laki 2 kwaajili ya kununuliwa kitoweo kwa kila kituo lengo nikuhakikisha wanarejesha tabasam kwa walengwa hao nikuhakikisha wanasherehekea sikuu ya Mwaka mpya.

“Tumefanya hili kwaajili ya kurejesha tabasam kwa ndugu zetu hasa makundi haya ya Wazee watoto waliokimbia ukatili Wazee na wenye mahitaji Maalum Sisi kama Taasisi tunahitaji kurejesha tabasam kwao nahii imekuwa nidesturi yetu”Alisema Modest Miachel Mratibu Nyansaho Foundation.
Wakizungumza baadhi ya wasimamizi wa vituo waliopokea msaada huo wameipongeza Taasisi ya Nyansaho kwa kuwakumbuka na kusema kuwa imekuwa taasisi inayojari na kuwakumbuka Wakati wote siwakati wa sherehe Pekee
