Watoto Zaidi ya 400 waliokuwa hatarini kushindwa kuanza masomo kidato cha Kwanza na Darasa la Kwanza kutokana na maisha duni katika Halmashauri ya Mji wa Bunda wamekabidhiwa Vifaa vya shule ili kuhakikisha wanaanza masomo.
Wakizungumza baadhi ya Wazazi na walezi wamepongeza hatua hiyo kwani inaonesha Upendo na kusaidiana wakati wa shida.

“Binafsi Mimi nilikuwa sina na sijui mwanangu anaendaje shule maana sina chochote maisha Yangu nafanya vibarua ndio nile kwahiyo nashukuru Sana Kwa msaada huu yaani sina chakusema”Dayana Marwa Marwa mkazi wa Bunda.
Vifaa hivyo vya shule vimetolewa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ambae pia nidiwani Wakata ya nyamakokoto Daud Miachel ambapo amesema watoto hao waliibuliwa kutoka katika familia Duni ambapo wasingesaidiwa wasingeweza kwenda shule kabisa
