Latest Posts

MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI UGANDA ADAI KUTISHIWA MAISHA

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, Simon Byabakama, amefichua kuwa amekuwa akipokea vitisho dhidi ya maisha yake vinavyomtaka atangaze wagombea mahususi kuwa washindi katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika kesho Alhamisi, Januari 15, 2026.

Akijibu swali la shirika la habari la BBC kuhusu klipu ya video inayomwonesha msaidizi mkuu wa Rais Yoweri Museveni akidai kuwa Tume hiyo haiwezi kamwe kumtangaza mpinzani Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) kama mshindi, Bw. Byabakama amesisitiza kuwa hofu haipo katika msamiati wake na atatangaza kile ambacho wapiga kura wameamua.

“Sheria ya Uchaguzi wa Rais inaagiza Tume kuhakikisha, kutangaza na kuchapisha matokeo ya uchaguzi. Huwezi kukwepa kifungu hicho cha sheria. Sifanyi kazi ya kuchangia kura; ni mpiga kura ndiye anayeamua, na kile ambacho wapiga kura wamesema ndicho nitatangaza kwa taifa,” amesema Bw. Byabakama kwa msisitizo.

Kauli hiyo inakuja baada ya video ya Msaidizi Maalum wa Rais, Bw. Yiga Kisakyamukama, kusambaa mtandaoni akisema: “Usitarajie wala usifikirie kwamba Byabakama anaweza kumtangaza Bobi Wine. Rais Museveni atasalia uongozini; usifikirie kuwa Museveni ataondoka madarakani kwa kupiga kura.”

Licha ya vitisho hivyo kutoka kwa watu aliowaita “wasiokuwa na kazi,” Mwenyekiti huyo amewahakikishia Waganda kuwa Tume iko huru na itazingatia kanuni za hesabu za kura pekee. Amesema Uganda itasalia kuwa nchi salama hata baada ya upigaji kura wa kesho, ambapo watu zaidi ya milioni 20 wanatarajiwa kuchagua Rais na Wabunge.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!