Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdurahaman, amesema kuwa fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, zinapaswa kuwafikia walengwa waliokusudiwa ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Tanga, Abdurahaman amesisitiza kuwa siyo sahihi kwa fedha hizo zinazolenga kusaidia vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kunufaisha watu wachache pekee, badala ya kuwafikia walengwa halisi waliokusudiwa.

Ameeleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi, huku akisisitiza uwajibikaji kwa watendaji wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo.
Aidha, Abdurahaman amesema hatoridhishwa na taarifa za makaratasi pekee, bali ataendelea kufika moja kwa moja katika maeneo husika ili kujionea utekelezaji wa miradi na maendeleo yaliyofikiwa kwa walengwa waliokusudiwa.