Latest Posts

CHALAMILA AZINDUA JENGO LA KISASA LA TAKUKURU IRINGA LA SHILINGI BILIONI 1.6

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila, leo amezindua jengo jipya la kisasa la ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Iringa lililojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Chalamila amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2026/2027, TAKUKURU inatekeleza miradi 12 ya ujenzi wa majengo ya ofisi za mikoa na wilaya, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi, kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa.

Naye Mkurugenzi wa Milki wa TAKUKURU, Mhandisi Dkt. Emmanuel Kiabo, amesema jengo hilo limejengwa kwa kuzingatia viwango vya kisasa. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daudi Yassin, ameipongeza TAKUKURU kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya rushwa na kuhamasisha ushiriki wa jamii katika vita dhidi ya rushwa.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi wa Serikali, Chama, taasisi mbalimbali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Iringa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!