Tukio hilo lilitokea saa tano asubuhi, wakati bibi harusi alikuwa anawasili ukumbini kwa ajili ya kubadilishana viapo na mchumba wake. Kabla hata hajashuka kwenye gari, mbwa hao watatu ambao walikuwa wakimilikiwa na jirani wa ukumbi huo walianza kulia kwa sauti tofauti na kawaida. Ghafla, mmoja wao alisema kwa sauti inayoeleweka: “Acha kuolewa, wewe si mchamungu.” Wenzake wawili wakaungana: “Tunapinga ndoa hii, bibi harusi ana roho ya uhasidi.”
Watu waliokuwa karibu walitawanyika kwa woga, wengine wakianguka chini kwa hofu, na baadhi walipoteza fahamu. Maisha ya sherehe yalibadilika kuwa taharuki ya ghafla, huku wazazi wa pande zote mbili wakibaki wamepigwa butwaa. Soma zaidi hapa.