Latest Posts

IGP WAMBURA AKAGUA UJENZI WA NYUMBA NA MABWENI SHULE YA POLISI MOSHI

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Camillus wambura akiambatana na maafisa wengine wa Polisi Makao Makuu Dodoma, wamefanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za wakufunzi na familia zao pamoja na ujenzi wa mabweni ya wanafunzi kwenye shule ya Polisi Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

Ujenzi huo unatekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa miundombinu ya ujenzi wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa ndani ya Chombo hicho cha ulinzi na usalama.

Kukamilika kwa miradi hiyo katika shule hiyo ya Polisi Moshi kunatarajiwa kuongeza morali katika utendaji kazi kwa Maafisa wa Polisi sambamba na kukuza ustawi wa askari kwa kukaa na kuishi kwenye mazingira bora na ya kisasa jambo litakalowawezesha kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi katika kuwalinda wao na mali zao.

Kando ya maboresho na ujenzi wa miundombinu, Kumefanyika pia maboresho katika mitaala ya mafunzo kwa Askari Polisi sambamba na Shule hiyo kuingia kwenye mikataba na vyuo vya ndani na nje ya nchi ili kuendana na utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Haki jinai iliyopendekeza askari Polisi kujengewa uwezo wa kitaaluma na utendaji kazi.

Kulingana na taarifa ya Polisi kwa Vyombo vya habari jana Februari 11, 2026, katika utekelezaji wa pendekezo hilo jumla ya askari 111 wamefanikiwa kuhitimu masomo katika ngazi ya uzamili (Masters) kwa mwaka 2025 kutokana na uwepo wa Tawi la Chuo cha uhasibu Arusha (IAA) katika shule hiyo ya Polisi Moshi, ambao wanaendesha kozi mbalimbali za kuwajengea uwezo na ujuzi Askari kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!