Katika hali ya kusikitisha na isiyo ya kawaida, mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Issa Ramadhani (35), mkazi wa Mtaa wa Mnyakongo, Kata ya Nkuhungu jijini Dodoma, anatuhumiwa kwa kubaka na kulawiti watoto watatu wenye umri chini ya miaka 3 na kuwasababisha majeraha makubwa sehemu zao za siri Kwa tukio hilo la kikatili ambalo ni kinyume na sheria za nchi.
Wakizungumza na JAMBO TV, wazazi wa watoto hao wamesema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 12 Agosti, majira ya saa tano asubuhi, wakati watoto hao walipokuwa wakicheza katika mazingira ya nyumbani ambapo Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliwadanganya watoto hao na kuwapeleka katika pagale lililopo karibu na mazingira hayo ambako aliwafanyia vitendo hivyo vya kikatili.
Baada ya tukio hilo, wazazi hao wamesema mtuhumiwa alikimbia kutoka eneo la tukio ndipo wazazi hao walipowachukua watoto wao na kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma (Central) kwa ajiri ya kuripoti tukio hilo na kupewa fomu ya matibabu (PF3) ili watoto hao wapatiwe huduma ya haraka ya kitabibu.
Aidha Wazazi wamesema kuwa vipimo vya kitabibu vilithibitisha kuwa watoto wao walilawitiwa na walipata majeraha katika sehemu zao za siri kutokana na ukatili huo.
Aidha Licha ya kuripoti katika kituo cha polisi na mtuhumiwa kukamatwa, wazazi hao wamelalamikia kucheleweshwa kwa mchakato wa kisheria, wakieleza kuwa hadi sasa hawajaitwa mahakamani kutoa ushahidi, na hawana taarifa rasmi kuhusu alipo mtuhumiwa pamoja na hatma ya kesi hiyo.
Ambapo wameiomba Serikali na vyombo vya dola kuchukua hatua kali ili kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mahakamani na haki inatendeka kwa lengo la kuzuia matukio kama hayo kutokea katika jamii.
Akizungumza na JAMBO TV, mmoja wa watoto hao aliye Bakwa na kulawitiwa amesema kuwa mtuhumiwa aliwadanganya kwa kuwaambia kuwa waende katika pagale kwani kuna makopo mengi ya kuchezea ndipo walipofika huko alianza kuwavua nguo na kuwafanyia vitendo hivyo ambapo mtoto huyo amesema  walipojaribu kupiga kelele, mtuhumiwa aliwatisha kuwa atawaachia mbwa wawashambulie.
JAMBO TV haikuishia hapo imemtafuta Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Mnyakongo, Bw. Stephano Chiwaligo ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mtuhumiwa ni mtu mwenye akili timamu, japo hutumia vilevi kama vile pombe, sigara na bangi.
Aidha Bw. Chiwaligo amesema ofisi yake inafuatilia kwa karibu mwenendo wa kesi hiyo na ameahidi kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa katika vyombo vya sheria ili haki iweze kutendeka huku aliwasihi wazazi na walezi kuwa makini zaidi katika kuwalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji vinavyoweza kujitokeza.