Latest Posts

KAMPENI YA KUTOKOMEZA ZERO MANISPAA YA MUSOMA YAANZA.

Shule ambazo zimefanya Vizuri katika mitihani ya Kitaifa, Manispaa ya Musoma Mkoani Mara zimetambuliwa na kupewa zawadi mbalimbali ikiwa ni motisha kuhakikisha walimu hao wanaendelea kufanya vizuri katika kampeni ya kutokomeza zero katika matokeo ya Kitaifa.

Kampeni hiyo ya kupambana dhidi ya kutokomeza Zero katika Manispaa ya Musoma imeanzishwa na Mkuu wa wilaya ya Musoma na ambapo Mbunge  wa Viti Maalum Mkoa wa Mara Agness Marwa ameanza kuunga juhudi hiyo kwa kutoa tuzo kwa walimu ambao masomo yao yamefanya vizuri.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo na vifaa hivyo leo februari 18,2026 iliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Musoma mkoani Mara mbunge huyo alisema wamekabidhi vifaa hivyo kama ehemu ya kutambua mchango wa klundi hilo lawalimu kwa kazi kubwa wanayoifanya.

‘Nimeanza na hili hapa katika manispaa ya Musoma na lengo langu zaidi nikuhakikisha nashirikiana na wadau kutatua changamoto za kielimu kuondoa tatizo la zero kwa mkoa wetu tunahitaji kurudi kama zamani katuika kufanya vyema katika matokeo ya kitaifa’Alisem Agness Marwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara.

Aksihiriki katika zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Musoma Juma Chikoka alisema kampeni ya kutokomeza zero itaenda sambamba katika mapambano dhidi ya Utoro kwa wanafunzi wote kuhakikisha zinachgukuliwa  hatua kali kwa wale watoto ambao wamekuwa wakishindwa kuhudhuria shule bila taarifa kwa muda mrefu.

Pia Chikoka amewataka watendaji kwenda kusimamia swala la chakula kikamilifu mashuleni na swla hilo nilalazimiza sila hiali katika mkoa wa wilaya ya Musoma.

Aidha Baadhi ya walimu akiwemo Gabriel Magita Mkuu wa shule ya Musoma Ufundi ambaye nimiongoni mwa waliopata tuzo na  hizo alisema  sasa zinaenda kuwa chacha ya kuongeza ufaulu lakini pia kuwakumbusha kuongeza nguvu katika mapambano ya kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!