Mwandishi wa Jambo Tv Fredrizzo Samson (mwenye Suit ya Kijivu) akiongozana na Wakili Msomi David Mwita na Familia ya Soya One Limited amepokea Tuzo ya Kampuni ya Uchimbaji madini ya Soya One Limited iliyotunukiwa usiku wa Tarehe 05 March 2026

Mwandishi wa Jambo Tv Fredrizzo aliteuliwa kuiwakilisha Kampuni hiyo akiambatana na baadhi ya staff wamemuwakilisha Mkurugenzi Chacha Soya katika usiku huo wa Tuzo za wanawake Wajasiriamali na wafanyabiashara Mkoa wa Mara “Tanzania Women chamber of Commerce” (TWCC) ambapo Mkurugenzi wa Kampuni ya Soya One Limited Ndg. Chacha Soya amekuwa nguzo muhimu sana kwa makundi mbalimbali katika kuhakikisha vijana na wanawake wanajipambania katika kukuza uchumi wao, Chacha Soya ambaye ndio mdhamini mkuu wa TWCC mkoa wa Mara amepokea Tuzo mbili ambapo moja ikiwa ni Tuzo ya Heshima na Pili ikiwa ni Tuzo ya Kampuni Soya One Limited katika kufanya vizuri sekta ya madini.

