Baraza kuu la usalama la Umoja wa Mataifa, leo Septemba 12, 2025.limepanga kupiga kura ya azimio la kuitambua Palestina kama Taifa huru bila kuhusika kwa Hamas.
‎Taarifa hiyo ya umoja wa Mataifa imetolewa wakati ambao Israel imekuwa ikikosoa bodi ya umoja wa matiafa kwa karibu miaka miwili sasa kwa kushindwa kulaani shambulizi la Hamas kwa Israel lililofanywa Oktoba 07, 2023 wakati azimio la Ufaransa na Saud Arabia likiwasilishwa bila utata.
‎Azimio hilo linalo tambulika kwa sasa kama “Azimio la New York” lenye lengo la kutafuta amani ya kudumu katika vita vya Israel na Palestina ambapo katika sehemu ya maelezo yake limesema “Hamas lazima iwaachie Mateka wote” na kwamba baraza kuu la umoja wa Mataifa linakemea shambulizi lililotekelezwa na Hamas dhidi ya Raia tarehe 7 mwezi Oktoba.
‎Pia azimio hilo limeitisha juhudi za pamoja ili kumaliza vita vya Gaza, kuwezesha upatikanaji wa amani na kumaliza ukaliaji wa kimabavu unaofanywa na Israel kwa Hamas.
‎Aidha azimio hilo lilikuwa tayari limeungwa mkono na umoja wa Falme za Kiarabu na kutiwa saini na nchi 17 ambazo ni wanachama wa umoja wa Mataifa.
‎Imefafanua kuwa ili kumaliza vita Gaza, Hamas yenyewe lazima ikomeshe sheria zake huko Ghaza na kuweka silaha zake chini ya mamlaka ya Palestina kwa kushirikisha juhudi za kimataifa kwa lengo na kutafuta uhuru wa Taifa.
‎Kura hiyo itautangulia mkutano wa umoja wa Mataifa utakao ongozwa na wenyeviti wawili kutoka Riyadh pamoja na Paris Septemba 22 Huko New York ambapo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliahidi Kuitambua Palestina kama Taifa huru.
‎Hata hivyo baadhi ya Mataifa kama Ujerumani yamesema yanaunga mkono Azimio Hilo, huku yakibainisha kuwa si wakati sahihi kuitambua Palestina kama Taifa huru.
‎Viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Baraza hilo Annalena Baerbock, amesema mashariki ya kati haihitaji migogoro mingi bali juhudi za kidiplomasia ili Kuifikia amani.