Latest Posts

MAANDAMANO YA KUPINGA SERIKALI MOROCCO YASHIKA SURA MPYA, KADHAA WAUAWA

Maandamano ya kupinga serikali nchini Morocco kufuatia hali mbaya ya huduma za umma yamegeuka kuwa ghasia siku ya Jumatano baada ya watu wawili kuuawa na maafisa wa polisi walipofyatua risasi dhidi ya kundi lililokuwa linajaribu “kuvamia” kituo cha polisi huko Lqliaa, karibu na jiji la pwani la Agadi.

‎Taarifa hiyo ni kwamujibu wa vyombo vya habari vya serikali nchini humo, vilivyoripoti kwamba kundi hilo lilivamia jengo la vikosi vya usalama na kulichoma moto, na kuvilazimu vikosi vya usalama kutumia silaha za moto kujitetea.

‎Maafisa wamesema uchunguzi wa kimahakama kuhusu tukio hilo umeanza, ikiwa ni ishara ya mwelekeo wa hatari zaidi katika maandamano ya kupinga serikali, ambayo awali yalianza kama mwito wa mageuzi ya haki ya kijamii.

‎Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imesema hadi sasa, zaidi ya watu 400 wamekamatwa na karibu300 wamejeruhiwa wakati wa maandamano.

‎Maandamano hayo yalianza siku ya Jumamosi, yakidai elimu na huduma bora za afya huku malalamiko makuu ikiwa ni taifa hilo la Afrika kujenga viwanja vya michezo kama maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Fifa 2030 na kupuuzia matatizo ya afya ya umma na elimu.

‎Maandamano hayo, yamechochewa na mitandao ya vijana nchini humo ya, Moroccan Youth Voice na GenZ 212, ambao ndio walitoa wito wa kuandamana.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!