Latest Posts

MADIWANI MBINGA DC WATAKIWA KUSIMAMIA FEDHA ZA MIRADI KIKAMILIFU

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wametakiwa kusimamia kikamilifu fedha za miradi zinazotolewa katika kata zao ili kuhakikisha zinaleta tija kwa wananchi ambapo kila kata imetengewa kiasi cha shilingi milioni 100 kwa ajili ya kutekeleza miradi viporo na ile ambayo haikukamilika katika bajeti zilizopita.

Maagizo hayo yametolewa katika kikao cha Baraza la Bajeti la halmashauri hiyo ambalo limefanyika tarehee 13/2/2026 ambapo rasimu ya bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni 57 imepitishwa rasmi. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mhe. Desderius Haule, amesema halmashauri ina jumla ya kata 29 na kwamba uamuzi wa kupeleka shilingi milioni 100 kwa kila kata unalenga kukamilisha miradi iliyoanza ili iweze kuwanufaisha wananchi kwa wakati.

Mhe. Haule amewataka madiwani kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo, akisisitiza kuwa usimamizi madhubuti utasaidia kuondoa malalamiko ya ucheleweshaji au ubadhirifu wa fedha za umma. Amesema ni wajibu wa kila diwani kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo katika maeneo yao na kutoa mrejesho sahihi kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisale Makoli, amesema halmashauri hiyo ni miongoni mwa halmashauri zinazofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato ya ndani. Ameeleza kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano mzuri kati ya watendaji na madiwani wa halmashauri hiyo.

Amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, halmashauri ilipangiwa kukusanya shilingi bilioni 12 za mapato ya ndani, lakini ilifanikiwa kuvuka lengo hilo na kukusanya shilingi bilioni 14. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2025/2026, halmashauri imepangiwa kukusanya shilingi bilioni 12, ambapo hadi sasa tayari imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 10.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!