Latest Posts

MAFUNDI UJENZI: TUNAKUFA NA TAI SHINGONI KISA HATUNA BIMA

Mafundi ujenzi mkoani Njombe wameiomba serikali kuangalia kundi hilo na waweze kupata bima za afya ili kuwa na uhakika wa maisha wanapokutana na changamoto kazini.

Wakizungumza na Jambo TV Baadhi ya mafundi akiwemo Victor Mahenge ambaye ni fundi rangi kutoka halmashauri ya mji wa Makambako pamoja na Maria Kionaomela kutoka mjini Njombe,wanasema Mafundi wamekuwa wakifanya mambo makubwa kwenye sekta ya ujenzi lakini wanakumbana na changamoto afya zao zinapoteteleka.

“Mafundi wengi tunapata changamoto kazini lakini inakuwa ni siri yetu ila tukipata bima zitatusaidia kwa maana hata tukipata shida kwenye ufundi itakuwa rahisi kupata huduma ya afya”amesema Mahenge

Kwa kuona umuhimu wa kundi hilo la vijana linalojishughulisha ili kukuza uchumi pamoja na maendeleo ya taifa,sekta binafsi zimeanza kutoa bima za afya kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha afya na kuwaletea maendeleo watanzania.

Derick Mmasi ni muwakilishi kutoka Magic Builders International Ltd mara baada ya kuwa na mkutano wa pamoja na mafundi wa mkoa wa Njombe amesema wanakwenda kutoa Bima kwa mafundi 500 ili kuwapa uhakika wa maisha.

“Kwa mwaka huu tunaenda kugawa bima kwa mafundi 500 kwa sababu ni jamii ambayo inafanya kazi katika mazingira hatarishi na mkakati wetu ni kuendelea kutoa bima zaidi ya 500″amesema Mmasi

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!