Latest Posts

MALAWI YAPIGA KURA KUCHAGUA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI

Raia wa Malawi leo Jumanne Septemba 16, 2025, wanapiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, uchaguzi unaotazamwa kama kipimo muhimu cha mustakabali wa nchi hiyo hususan katika mapambano dhidi ya rushwa na ustawi wa uchumi.

Katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea 17 kutoka vyama mbalimbali wanashindana, huku ushindani mkubwa ukitarajiwa kati ya Rais wa sasa, Lazarus Chakwera, na mpinzani wake wa muda mrefu, Rais wa zamani wa nchi hiyo Peter Mutharika. Hii ni mara ya tatu kwa wawili hao kukutana kwenye kinyang’anyiro cha urais.

Wachambuzi wa siasa wameeleza kuwa safari hii Rais Chakwera anakabiliwa na upinzani mkali zaidi, hasa kutokana na changamoto za uchumi na athari za mabadiliko ya tabianchi. Katika kampeni zake, Chakwera aliahidi kukamilisha miradi aliyoianzisha, ilhali mpinzani wake Mutharika, mwenye umri wa miaka 85, ameweka kipaumbele katika kurejesha uchumi imara na kuimarisha uongozi ambao anadai umeyumba chini ya utawala wa sasa.

Mbali na wawili hao, wagombea wengine kama aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Dalitso Kabambe, wanaelezwa kuwa na nafasi ya kusababisha uchaguzi huo kuingia duru ya pili iwapo hakuna mgombea atakayepata zaidi ya asilimia 50 ya kura.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!