Latest Posts

MAOMBI YAFANYIKA NGORONGORO KUPUNGUZA MIGOGORO YA ARDHI

Vikao vya maombi vilivyohusisha jamii kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ngorongoro, vimefanyika katika Kijiji cha Kirtalo, Kata ya Soitsambu, Tarafa ya Loliondo, kwa lengo la kuliombea eneo hilo ili kupungua kwa migogoro ya ardhi inayoendelea kujitokeza.

Jamii hizo zimeeleza kuwa chanzo kikuu cha migogoro hiyo ni msukumo wa kubadilisha matumizi ya ardhi ya jamii, hali inayosababisha kuanzishwa kwa matumizi yanayokinzana na shughuli za kijamii na kiuchumi za wakazi wa eneo hilo, hususan kuanzishwa kwa hifadhi na miradi ya uwekezaji.

Katika vikao hivyo vya maombi, washiriki walisisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo ya wazi, ushirikishwaji wa jamii katika maamuzi, pamoja na kuheshimiwa kwa haki za ardhi ya kimila, hatua ambazo wameeleza kuwa ni msingi wa kudumisha amani na mshikamano wa wananchi.

Aidha, walitoa wito kwa Serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa maamuzi yanayohusu matumizi ya ardhi yanazingatia maslahi ya wananchi, ili kulinda maisha, utamaduni na shughuli za uzalishaji za jamii za wafugaji na wakazi wa Loliondo kwa ujumla.

Jamii hizo zimeeleza matumaini kuwa kupitia maombi, mshikamano wa kijamii na mazungumzo ya amani, maridhiano yataendelea kuimarika na amani kudumishwa katika Wilaya ya Ngorongoro.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!