Latest Posts

MARUFUKU VYUO VIKUU KUTOA PhD YA HESHIMA KWA WANASIASA ETHIOPIA

Wizara ya Elimu nchini Ethiopia imetoa agizo na mwongozo kwa vyuo ambavyo havitoi Shahada ya Uzamivu kuacha mara moja kutunuku shahada za heshima (Honorary Doctorate) kwa viongozi wa kisiasa nchini humo.

Tovuti ya Birr Metrics imeripoti kuwa mwongozo huo umetiwa saini na Waziri wa Elimu nchini humo Prof.Berhanu Nega na kuwasilishwa kwa taasisi za elimu ya juu hasa vyuo vikuu ambavyo wanafunzi wake hawana awamu nne na havitoi shahada ya uzamivu haviruhusiwi kutotunuku shahada ya heshima.

Aidha Wizara hiyo imefafanua kuwa shahada ya heshima inaweza kutolewa kwa raia wa Ethiopia au wa kigeni au kikundi cha watu ambao wametoa mchango wa kitaaluma nchini humo huku wafanyakazi wa serikali na viongozi wakiwa hawaruhusiwi kupokea tunu hiyo ikiwa bado wapo kazini hadi watakapomaliza utumishi wao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!