Latest Posts

MBETO: AMANI NA UMOJA FUNGUO ZA MILANGO YA MAENDELEO

Chama Cha Mapinduzi kimesema hakitaacha kuzihimiza  Serikali  zake zizidishe  mkazo na kuhakikisha hakuna  mtu au kikundi chochote  kinachoweza  kuvuruga Amani na Umoja.

Vile vile chama hicho kimefichua siri ya kupatikana   kwa maendeleo ya haraka  katika Awamu ya Nane Zanzibar  ni kuwepo kwa Ustawi wa  Amani na Utulivu .

Hayo yamebainishwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar,   Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo, Khamisi  Mbeto Khamis,  aliyesema  nchi  ikiwa katika mazingira ya Umoja ,milango ya   neema ya Maendeleo  hufunguka.

Mbeto  alisema inapokosekana Amani , Mshikamano na Utulivu , Serikali haiwezi kujenga  miradi  mikubwa kama ya Madaraja, Maji, Shule, Barabara, Bandari, Viwanja vya  Ndege , Michezo na  Masoko.

Alisema kwa muktadha huo  ,CCM imekuwa ikizielekeza  mara  zote  Serikali  zake zihakikishe hachekewi  mtu yeyote atakaethubutu kuvuruga tunu za   Amani na Umoja wa Kitaifa .

Pia Mbeto  alitaja kufanikiwa kwa  ujenzi  wa miradi ya maendeleo,  kumechochewa zaidi  na kasi ya ukusanyaji  Mapato kwa umakini kulikofanikisha kujenga miradi yenye tija.

“Serikali  ya CCM  Awamu  ya Nane Zanzibar  imejitahidi mno kukusanya mapato .Si hivyo  tu lakini pia imesimamia nidhamu ya matumizi ya fedha. SMZ sasa inakopesheka mahali kuliko wakati  wowote “Alieleza

Hata hivyo  katika maelezo yake   Mbeto alisema SMZ  hivi   sasa ina kibali cha uaminifu  wa kukopa katika taasisi zozote za fedha na kwenye benki zote.

‘Tunaingia kwenye  mbio za Uchaguzi  huu tukiwa na mategemeo makubwa  ya kushinda.Mgombea wetu Rais Dk Mwinyi ni kiongizi mchapakazi , muaminifu na mzalendo  “Alisema .

Katibu huyo  Mwenezi  aliwahakikishia wananchi kuwa ushindi utakaopatikana katika ngwe ya pili,utazidi kutanua wigo wa maendeleo yatakayowashangaza wengi Afrika Mashariki .

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!