Latest Posts

MILIONI 28.4 ZATUMIKA KUKAMILISHA MAABARA YA SAYANSI SHULE YA SEKONDARI LANGWA – TABORA

Maisha ya elimu yamechukua mwelekeo mpya katika Shule ya Sekondari Langwa baada ya kukamilika kwa ukarabati na umaliziaji wa maabara ya kisasa ya sayansi kwa gharama ya shilingi milioni 28.4.

Mradi huu umewezeshwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa kushirikiana na UNICEF, kupitia ufadhili wa Serikali ya Canada

Matokeo chanya tayari yameanza kuonekana ambapo, ufaulu katika masomo ya sayansi umeongezeka kwa asilimia 94% huku somo la Biolojia likiongoza kwa ufaulu, likifuatiwa na Kemia na Fizikia. Aidha, idadi ya wanafunzi wanaochagua kusoma masomo ya sayansi imeongezeka maradufu shuleni hapo.

Kupitia mradi huo, sasa wanafunzi wana uhakika wa kusoma masomo ya sayansi kwa vitendo, jambo ambalo limeongeza ari ya kujifunza kwa wanafunzi na motisha kwa walimu.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwa kushirikiana na UNICEF inaendelea kutekeleza miradi yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 2.5 katika mikoa ya Tabora, Kigoma na Songwe. Miradi hiyo inalenga kuinua ubora wa elimu, kupanua wigo wa fursa za kujifunza, na kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu bora bila ubaguzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!