Latest Posts

MIPAKA KUFUNGULIWA NA KUPUNGUZWA KODI KWACHOCHEA BIASHARA MTWARA

Kupunguzwa kwa viwango vya kodi kwa baadhi ya bidhaa, kuwepo kwa misimu mbalimbali ya mazao pamoja na kufunguliwa mipaka ya Msumbiji na Tanzania kumeamsha kasi ya biashara mkoani Mtwara.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Mtwara (JWT) tawi la Mtwara Hamza Licheta, amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wafanyabiashara katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa mujibu wa Licheta, awali mkoa wa Mtwara ulikuwa unategemea msimu mmoja tu wa zao la korosho  ambao haukuwa rafiki kwa wafanyabiashara hata hivyo, kuanza kupitisha bidhaa zote za wakulima na wafanyabiashara kupitia Bandari ya Mtwara kumeufanya mkoa huo kupata sura mpya kibiashara na kufungua milango mipya ya uwekezaji.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Selemani Kadege,amesema changamoto kadhaa ambazo wafanyabiashara walikuwa wakikumbana nazo sasa zimetatuliwa na  miongoni mwa changamoto hizo ni kusitishwa kwa kufungwa kwa maduka na maeneo ya biashara kiholela na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) bila kibali cha Kamishna, pamoja na kusitishwa kwa ufungaji holela wa akaunti za benki za wafanyabiashara na kuchukua fedha bila idhini.

Aidha, amesema kuwa serikali imetunga sheria ya kuzuia wageni kujihusisha na biashara zinazostahili kufanywa na wazawa, sambamba na kupunguza wingi na viwango vya tozo za OSHA.

Kwa upande wake Mjumbe wa Jumuiya hiyo Zabibu Dingumbi, ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kuwapigania wafanyabiashara na kuhakikisha wanafanya shughuli zao kwa amani, huku ikijenga urafiki kati ya wafanyabiashara na TRA

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!