Latest Posts

MITI 500 YA MATUNDA NA KIVULI KUSTAWISHA MAZINGIRA SHULE YA KIRIMA

 

Shule ya Sekondari Kirima iliyopo Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro imepanda jumla ya miti 500 rafiki wa mazingira katika kutekeleza kaulimbiu ya soma na mti.

Akizungumza Agosti 28,2025 katika zoezi hilo la upandaji wa miti,Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Regius Kagusha amesema kuwa jumla ya miti 500 imepandwa ikiwemo miti 300 ya matunda na miti 200 ya kivuli.

“Changamoto tuliyokuwa nayo katika Shule yetu ni kuwa na miti mingi ya kivuli pasipo kuwa na miti ya matunda,kilio hiki kimesikika baada ya Kampuni ya Bonite bottlers kutuwezesha miti ya matunda na sasa changamoto hiyo hakuna tena hivyo miti iliyopandwa tutaitunza kwa manufaa ya Wanafunzi na Jamii ya Kirima” Kagusha

Akizungumza kuhusu mazingira na kutunza miti hiyo Makamu Mkuu wa Shule hiyo, akimwasilisha Mwalimu wa mazingira Naomi Urio amesema kuwa wanayo rasilimali zote za kutunza miti hiyo ikiwemo maji ya mifereji na mto uliyokaribu na Shule hiyo pamoja na nguvu kazi ya Wanafunzi na walimu in hivyo miti hiyo kustawi na kutoa matunda kama ilivyo kusudiwa.

Kwa upande wake Leonard Makule Mratibu wa masoko kutoka Kampuni ya Bonite bottlers ameshukuru uwepo wa kaulimbiu ya shule hiyo ya soma na mti hivyo kuwataka Wanafunzi na uongozi wa shule hiyo kusimamia miti iliyotolewa na kupandwa ili wafaidi matunda,kivuli na mazingira yaliyoboreshwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!