Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi amesema mkoa huo unatarajia kupanda miti Milioni 13 katika Halmashauri zote za mkoa huo ikiwa ni mkakati wa utunzaji wa mazingira.
Mkuu huyo wa mkoa ameyasema hayo Leo Januari 14,2026 aliposhiriki zoezi la upandaji miti kupitia Kampeni ya Mti wa Mama maarufu kama 27 ya Kijani inayoendeshwa na Shirika la Utangazaji (Tbc) kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)

Kanali Mtambi amesema mkoa umeelekeza kila Halmashauri kupanda miti Milioni moja na nusu ambapo kwa mwaka jana jumla ya miti Milioni saba (7) ilipandwa.
Ameitaja Halmashauri ya Serengeti kufanya vizuri na kuongoza katika kupanda miti kwani hadi kufikia sasa tayari wamepanda miti Milioni moja na laki mbili.
Amewataka Wananchi mkoani humo kujenga mazoea ya kupanda miti katika maeneo yao badala ya kungoja maelekezo kutoka kwa Wadau na Serikali.