Latest Posts

MKAKATI MAALUMU KUUNDWA KUIUNGANISHA ZANZIBAR NA ARUSHA ZINUFAIKE ZAIDI KIUTALII

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii visiwani Zanzibar Hafsa Mbamba amesema kupitia makubaliano ya awali yaliyosainiwa Kati ya Zanzibar na Tanzania bara kunatarajiwa kuundwa mkakati maalumu wa kuiunganisha Zanzibar na Arusha ili kunufaika zaidi na sekta ya utalii yenye kuiingizia nchi fedha nyingi za kigeni.

Mbamba ametoa kauli hiyo Jumamosi Juni 08, 2024 ikiwa ni siku ya pili ya maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 yanayofanyika Mjini Arusha kwenye viwanja vya Magereza na kusema kuwa makubaliano hayo yatasaidia kubadilisha watalii na wageni mbalimbali kati ya pande hizo mbili muhimu za muungano hasa katika kuutangaza na kuvutia utalii uliopo nchini Tanzania.

Mbamba amesema makubaliano hayo kati ya Zanzibar na Tanzania bara yatasaidia kuimarisha mashirikiano ya pamoja na kuchagiza jitihada za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  na Dkt. Hussein Mwinyi wa Zanzibar ambao wamekuwa wakiutangaza utalii wa Tanzania kupitia filamu mbalimbali.

Katika hatua nyingine Mbamba ametangaza ujio wa maonesho makubwa ya kimataifa ya utalii visiwani Zanzibar yatakayofanyika Oktoba 25- 26 ikiwa ni sehemu ya mageuzi makubwa ya sekta ya utalii visiwani Zanzibar yenye lengo la kubaini na kuendeleza vivutio vingine vya utalii kando ya utalii wa fukwe ulio maarufu visiwani humo.

Mbamba pia amezungumzia namna walivyofanikiwa kuwafanya Wazanzibar wote kufahamu vivutio vya utalii vilivyopo Zanzibar na kusema kuwa wamekuwa na mkakati wa kufundisha vivutio hivyo kuanzia shuleni, kutoa mapunguzo ya viingilio vya kuingia hifadhini na wakati mwingine kutokuweka viingilio pamoja na kuwa na bajeti ya kuelimisha jamii kuhusu utalii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!