Mariam alizaliwa katika familia maskini huko Taita Taveta. Baba yake alifariki akiwa mdogo, na mama yake alibaki akihangaika kulea watoto wanne kwa kuuza mboga sokoni. Kwa sababu ya ukosefu wa karo, Mariam alilazimika kuacha shule akiwa kidato cha pili. Hapo ndipo akaamua kutafuta kazi yoyote ya kuisaidia familia yake.
Bahati haikuwa yake sana mwanzoni. Alipata kazi ya kuwa haushelp kwa familia moja jijini Nairobi. Kila siku alikuwa anaamka saa kumi alfajiri kupika, kufua, na kusafisha nyumba kubwa ambayo ilimchosha hata zaidi kuliko ualimu wa shule yake ya sekondari. Mshahara wake ulikuwa mdogo mno, lakini Mariam hakukata tamaa. Alijua ni bora afanye kazi hiyo kuliko kurudi kijijini mikono mitupu. Soma zaidi hapa.