Latest Posts

MTIKISIKO IRAN: MAELFU WAINGIA MITAANI KUDAI MAPINDUZI, INTANETI YAZIMWA TAIFA ZIMA

Maandamano makubwa ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mingi yameikumba Iran, huku maelfu ya wananchi wakimiminika mitaani katika mji mkuu Tehran na miji mingine zaidi ya 100.

Video zilizothibitishwa zinaonesha waandamanaji wakidai mabadiliko ya mfumo wa utawala, huku wakitoa wito wa kurejeshwa kwa Reza Pahlavi, mtoto wa Shah wa zamani wa Iran anayeishi uhamishoni nchini Marekani.

Licha ya maandamano ya Alhamisi kuanza kwa amani bila kuingiliwa na vikosi vya usalama, hali imekuwa ya wasiwasi baada ya mashirika ya haki za binadamu kuripoti vifo vya makumi ya watu, wakiwemo watoto.

Shirika la HRANA limekadiria kuwa takriban waandamanaji 34 wameuawa, huku shirika la IHR likitaja idadi kubwa zaidi ya watu 45. Kwa upande wake, serikali ya Iran imepunguza uzito wa maandamano hayo, ikionesha picha za mitaa tupu huku ikidhibiti kwa kiasi kikubwa huduma ya intaneti nchini kote kupitia kile kinachoitwa “kuminya uhuru wa kidijitali.”

 

Hasira ya wananchi imechochewa na kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya nchi hiyo, na sasa yamefikia siku ya 12 mfululizo. Reza Pahlavi, ambaye amewapongeza waandamanaji kama “watu wajasiri,” ametoa wito wa kuendelea kwa maandamano hayo huku akimshukuru Rais wa Marekani Donald Trump kwa shinikizo lake dhidi ya utawala wa Tehran.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!