Latest Posts

MUFTI: TUSIKUBALI VIASHIRIA VINAVYOWEZA KUVUNJA AMANI, NCHI SIYO YA SERIKALI

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Bin Zubeir Ally, amewataka Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, maadili na ustawi wa jamii, hasa katika kipindi hiki ambapo Taifa linaelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.

Akizungumza mbele ya waumini wa Kiislamu katika Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma, Sheikh Dkt. Abubakar amesema amani ndiyo msingi wa Uislamu na chachu ya maendeleo ya jamii yoyote, akisisitiza kwamba Waislamu wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha utulivu, mshikamano na maadili vinaendelea kudumishwa nchini.

Aidha, kiongozi huyo wa dini amezungumzia changamoto ya mmomonyoko wa maadili unaoikabili jamii, akibainisha kuwa malezi ya watoto katika misingi ya dini na maadili ya taifa ndiyo ngao pekee ya kulinda kizazi kijacho dhidi ya athari hizo.

Amewataka wazazi na walezi kuwalea watoto wao kwa misingi ya dini, heshima na upendo ili kulinda tunu za Taifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Denis Masanja, amewataka wananchi wote wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi mkuu ili kutimiza haki yao ya kikatiba.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!