Latest Posts

MZEE MWANDAMBO ACHOSHWA NA WANAHARAKATI “NI WAONGO NA WAZUSHI”

Mtanzania na mtengeneza maudhui ya Mtandaoni kutoka Mkoani Mbeya Bw. Clemence Mwandambo ameshangazwa na kukemea tabia za propaganda na wale wote wanaoeneza taarifa potofu katika mitandao ya Kijamii ikiwemo zile zinazowahusisha Viongozi wakuu wa serikali na Vyombo vya ulinzi na usalama.

Mwandambo amebainisha hayo Alhamisi Machi 05, 2026 kupitia mitandao yake ya Kijamii, akihoji sababu za kufanya hivyo, ikiwemo uzushi wa vifo na kuwahusisha Viongozi wa serikali akiwemo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na familia yake.

“Hii dunia ina watu wa ajabu sana. Kuna kipindi baadhi ya watu wakavumisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amefariki, yaani mtu anajigamba kuwa yeye ni jasusi na ana taarifa na siri za Ikulu na kutuaminisha kuwa Rais hayupo na hamtamuona tena, baadaye Rais alipojitokeza hadharani hata kuomba radhi hawakuomba. Ninachoka mimi Mzee wenu, hizi Propaganda za nini Watanzania? Kwanini tunafanya hivi?” Amehoji Mzee Mwandambo.

Mwandambo amezungumzia pia madai ya baadhi ya watu kuihusisha Meli ya FMS Eagle iliyokamatwa nchini El Salvador ikiwa inapeperusha bendera ya Tanzania na ikiwa na shehena ya dawa za kulevya, akishangazwa na baadhi yao kuhusisha dawa hizo za kulevya na mtoto wa Rais Samia.

Akizungumza na BBC kuhusu tukio la Meli hiyo, Mhe. Hamza Hassan Juma, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa rais Zanzibar, alisema, “hakukuwa na raia wa Tanzania katika meli iliyokamatwa El Salvador, wala sio meli ya Tanzania, na haimilikiwi na Tanzania na Tanzania haihusiki na biashara ya dawa ya kulevya.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!