Nilikuwa mfanyakazi wa kawaida kwenye kampuni ya kusafisha maofisi, nikilipwa mshahara wa kutosha tu kula na kulipa kodi. Niliwahi kujiwekea lengo la kununua kiwanja, lakini kila nikianza kuweka akiba, jambo la dharura linatokea mtoto anaugua, shule zinadai karo, au vifaa vya nyumbani vinaharibika. Miaka ilivyopita, nilianza kuamini labda umiliki wa nyumba ni kwa wale waliozaliwa katika familia zenye uwezo au waliobahatika kuolewa na watu wenye mali.
Kuna kipindi niliishi kwenye nyumba ya vyumba viwili na watoto watatu. Majirani walikuwa na kelele kila usiku, na kila asubuhi ningeamka na harufu ya choo kwa sababu mifereji ilikuwa imejaa. Nililia sana kimoyomoyo, si kwa sababu ya hali yenyewe, bali kwa sababu ya kutokuwa na tumaini la kuibadilisha. Nilikuwa mvivu wa hata kuota ndoto. Maisha yalikuwa tu ni kesho nyingine ya kupambana. Soma zaidi hapa.