Latest Posts

POLISI WA KENYA DHIDI YA MATATIZO YA GENGE HAITI, ‘MAENDELEO YAMEKUWA MADOGO’

Miezi miwili baada ya maafisa wa polisi wa Kenya kufika nchini Haiti, maendeleo dhidi ya magenge hatari nchini humo yanaonekana kuwa madogo na maendeleo ya mpango wa kimataifa wa ulinzi yanaonekana kuwa yamekwama.

Kwa msaada wa Umoja wa Mataifa na ufadhili kutoka Marekani, mpango huu ulikuwa unatarajiwa kuleta utulivu katika taifa ambapo makundi ya silaha yanadhibiti asilimia 80 ya mji mkuu, Port-au-Prince.

Kwa mujibu wa The Citizen Digital, polisi wa Kenya wanaokisiwa kuwa 400 na wenzao wa Haiti hawajachukua tena ngome za magenge, hali ambayo imesababisha kero kubwa miongoni mwa wakazi wa jiji.

“Vikosi vya magenge vinaendelea kututesa, na wahalifu hawa hawana wasiwasi,” alisema dereva wa bodaboda, Watson Laurent (39) alipoongea na Shirika la Habari la AFP ambapo ameeleza kuwa aliwakuwa na imani na mpango huo wa kurejesha amani Haiti.

Haiti ilizama katika machafuko zaidi baada ya kuasi kwa magenge yaliyoratibiwa mnamo Februari, ambayo yalishambulia uwanja wa ndege wa kimataifa na vituo vya polisi, na kusababisha kujiuzulu kwa waziri mkuu Ariel Henry.

Mpango wa Uungaji Mkono wa Usalama wa Kimataifa (MSS), ambao Kenya ilikuwa imechukua jukumu la kuongoza ulikuwa tayari umeandaliwa na hatimaye ulitekelezwa ili kusaidia Haiti kukabiliana na hali ya kutisha ya usalama.

Wakenya wa kwanza 200 walifika mwishoni mwa mwezi Juni huku wengine 200 wakifika mwezi Julai, hata hivyo baadhi ya wachambuzi akiwamo Diego Da Rin anayetoka katika shirika la kimataifa la Crisis Group ameonesha wasiwasi wake juu ya uwezo na umahiri wa vifaa vya jeshi la Kenya kwenye kuanzisha operesheni za mashambulizi halisi dhidi ya magenge.

Wakenya na Polisi wa Taifa wa Haiti wamelinda majengo muhimu na vituo katika mji wa Port-au-Prince, huku magenge yanayoshutumiwa kwa ubakaji, mauaji na utekaji nyara, yakishikilia maeneo yao kwa kiasi kikubwa.

Operesheni kuu pekee ambayo polisi wa Kenya walihusishwa nayo ilikuwa mwishoni mwa mwezi Julai, wakati genge la Mawozo lilipochukua mji wa Ganthier, kilomita 28 mashariki mwa Port-au-Prince.

Lakini kabla ya vikosi vya usalama kufika, wanachama wa genge walikimbia mji huo na baadaye kurejea kuuteka mara baada ya polisi wa Kenya na Haiti kuondoka.

Polisi wa Kenya wamesema wamepiga maendeleo makubwa ikiwa ni pamoja na kusaidia kurejesha miundombinu muhimu kama uwanja wa ndege uliokuwa chini ya udhibiti wa magenge.

Kuibuka kwa magenge ya waasi kuliibua wasiwasi mkubwa katika nchi inayokumbana na migogoro ya kisiasa, majanga ya asili na umaskini.

Takribani watu 600,000 wamehamishwa nchini Haiti, kulingana na Umoja wa Mataifa huku takriban milioni 4.5 wakikosa chakula cha kutosha.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!