Jeshi la Polisi mkoani Mara limewataka viongozi wa Baraza la wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Bawacha kusistisha mpango wao wakufanya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani march8,2026 mjini Musoma badala yake kufata amri ya mahakama yakutokufanya shughuli za kisiasa hadi hadi kesi yao ya msingi itakapomalizika mahamani.
Kamanda wa polis mkoa wa Mara pius Lutumo akizungumza na wandishi wa habari amesema wameona picha mjongeo za BAWACHA kwenye mitandao ya kijamii zikihamasiaha kufanya maadhimisho ya siku ya wanawake 08-3-2026 kufanya hivyo nikukiuka kwa makusudi amri ya mahamakama.
Hivyo jeshi la polisi mkoani Mara limewataka viongozi wa BAWACHA waliofanya kikao cha maandalizi kufika ofsi ya mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Mara makosa ya jinai march 2-2026 kwa mahijiano.
“Jeshi la polisi linaendelea kutambua amri hiyo kwani haijtenguliwa kwa maana hiyo tunawashauri CHADEMA kurudi mahakamani kumalizi shauri lao badala ya kukaidi amri ya mahakama ambayo kimsingi nidharau kwa mahakama (Contempt of court) “Alisema kamanda wa polisi mkoa wa Mara Pius Lutumo. 