Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Alexander Mkumbo amehutubia katika kongamano la “Thought Leadership on China-Africa Trade and Investment Forum” lililoandaliwa na Benki ya Viwanda na Biashara ya China jijini Beijing.
Â
Kongamano hilo ni sehemu ya shughuli zinazofanyika kando ya mkutano wa FOCAC (Forum on China-Africa Cooperation) na linalenga kuhamasisha uwekezaji katika sekta za miundombinu, madini, nishati, na kilimo katika nchi za Afrika.

Â
Kongamano hili limehudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi waalikwa, mawaziri, maafisa waandamizi, pamoja na wawekezaji na taasisi za kifedha za kimataifa.
Â
Katika hotuba yake, Prof. Mkumbo alipata fursa ya kueleza kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania. Aidha, ujumbe wa Tanzania ulipata nafasi ya kukutana na wawekezaji wakubwa kutoka sekta za miundombinu, madini, nishati, na kilimo.
