Latest Posts

PUTIN AMSIFU TRUMP KABLA YA MAZUNGUMZO MAKUBWA

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesifu juhudi za dhati za Marekani za kutaka kumaliza vita nchini Ukraine, saa chache kabla ya kukutana na Rais Donald Trump katika mkutano wa kilele unaofanyika leo jimboni Alaska.

Kwa mujibu wa DW, Putin alitoa kauli hiyo alipokutana na mawaziri waandamizi na maafisa wa usalama, akieleza matarajio kwamba mazungumzo hayo yanaweza kutoa mwanga mpya wa kumaliza vita vikubwa zaidi barani Ulaya tangu Vita ya Pili ya Dunia.

Rais Trump amesema ana matumaini kuwa Putin yuko tayari kukomesha vita vyake nchini Ukraine, lakini ameonya kuwa makubaliano yoyote ya amani yanaweza kuhitaji mkutano mwingine utakaomshirikisha Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.

Zelensky na viongozi wa Ulaya wameongeza jitihada mapema wiki hii kuhakikisha hakuna makubaliano yatakayoiweka Ukraine pembeni, wakisisitiza kulindwa kwa maslahi ya taifa hilo katika mazungumzo yajayo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!