Wafanyabiashara wadogo wa mnadani (Machinga) mkoa wa Njombe,wamesema kufunguliwa kwa mnada kwenye mji wa Njombe kumefungua njia ya mafanikio yao kutokana na kilio cha muda mrefu kwa serikali iwasaidie eneo kwa ajili ya biashara.
Omary Kisangaike ni mmoja wa wajasiriamali,akiongea na Jambo TV wakati wa ufunguzi wa mnada Njombe mjini jana February 17,amesema walikuwa wakiomba muda mrefu kupata eneo bila mafanikio lakini kwa sasa wanaamini biashara yao inakwenda kukua.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete ametumia nafasi hiyo kukaribisha wawekezaji kwa kuwa mji huo ni rafiki kwa uwekezaji.

“Ni wahamasishe ndugu zetu waliopo Njombe na nje kuja Njombe kuwekeza ikiwemo ujenzi wa hotel”amesema Mpete
Akifungua Mnada huo Mkuu wa Wilaya ya Njombe Juma Sweda,ametaka wajasiriamali hao kuongeza nguvu ya kutafuta fedha kwa kuwa serikali inaendelea kuwajengea mazingira rafiki kwa shughuli zao