
Menejimenti ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi Bw. Masozi Nyirenda Agosti 15, 2024 wamekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUTI) cha Jijini Mwanza Balozi Profesa Costa Mahalu katika Ofisi za TEA Jijini Dodoma.
Katika kikao hiko, Balozi Profesa Mahalu aliongozana na Rev. Profesa Emmanuel Wabanhu ambapo walijadiliana mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu, pamoja na namna ya kuboresha mahusiano baina ya SAUTI na TEA na kushirikiana katika kuongeza ubora wa elimu.
Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUTI) ni moja kati ya taasisi zilizonufaika na miradi mbalimbali ya uboreshaji miundombinu ya elimu inayotekelezwa na TEA kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.