Latest Posts

TUIJENGE NCHI YETU KWA PAMOJA NA KUOMBEA AMANI IDUMU- KIROBA

Adam Kiroba, Mkazi wa Mkera, Chanika, Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam,  amewataka watanzania hususani Vijana kote nchini kudumisha amani, mshikamano na upendo kwenye jamii na kujiepusha na vurugu na uvunjifu wa amani kwani mara zote waathirika wakubwa wa vurugu mara zote wamekuwa akinamama, Watoto, Wazee pamoja na wale wasiokuwa na hatia kutoka kundi la wananchi wenye kipato cha chini.

“Mimi ninachowaomba watanzania ni kuwa nchi yetu inasifika kuwa kisiwa cha amani, tuendelee na sifa hiyo kwasababu machafuko ya juzi athari zake tumeziona na wengine mpaka leo biashara na sehemu za kuishi hawana. Niwasihi watanzania wenzangu tudumishe amani iliyopo na tusiwe sehemu ya kuhamasisha hicho kinachoendelea na tuwe wavumilivu na kuangalia namna ya kuijenga nchi yetu.” Amesisitiza Bw. Kiroba.

Bw. Kiroba akizungumza na mwandishi wetu wa habari leo Jumapili Novemba 09, 2025 amewataka pia Vijana kutofuata mikumbo kutoka kwa baadhi ya watu, akiwahamasisha pia wale wote wenye kuamini katika Mungu kupitia dini zao na madhehebu mbalimbali kuendelea kuiombea nchi ya Tanzania ili amani, umoja na mshikamano viendelee kudumu kwa maslahi ya kila Mtanzania.

Amesisitiza pia umuhimu wa kutambua faida za amani kwenye jamii, akisema ghasia na vurugu za Oktoba 29, 2025 kumewagharimu pia watu wasiokuwa na hatia, kusababisha ugumu wa upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii pamoja na kupanda kwa gharama za maisha na kuyumba kwa uchumi kwa watu wengi wa kipato cha chini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!